Wadau wa zao la Parachichi nchini wameiomba Serikali iendelee kuboresha mazingira ya ukuaji wa zao hilo kuazia kwenye kilimo hadi sokoni, ili Wakulima wanufaike na zao nalo.
Wadau hao wametoa ombi hilo mkoani Iringa wakati wa kongamano la Wadau wa Parachichi ambapo akifungua kongamano hilo Mkuu wa mkoa huo Queen Sendiga amesema Serikali inatatua changamoto za Wakulima wa Parachichi kwa awamu, na kuwataka Wakulima kuzingatia ubora ili kushindana kwenye soko la Kimataifa.