Mzunguko wa 16 bora ligi ya mabingwa barani Ulaya unaendelea leo usiku, vinara wa ligi kuu England timu ya Manchester City itashuka dimbani kuwakaribisha Sporting CP ya Ureno katika mchezo wa marejeano ambapo mchezo wa awali Manchester City waliibugiza Sporting mabao 5 kwa nunge
Huko katika dimba la Santiago Bernabeu timu ya Real Madrid itawakaribisha Paris Saint-Germain (PSG) ya Ufaransa kucheza mchezo wa marejeano mchezo unaotarajiwa kuwa wakuvutia na kusisimua baada ya Paris Saint-Germain (PSG) kushinda bao moja kwa bila nyumbani sasa ni zamu ya Real Madrid kutumia faida ya kucheza nyumbani ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele katika michuano hiyo mikubwa ya vilabu barani Ulaya
Michezo mengine usiku wa leo ni mechi 2 za ligi ya Europa mzunguko wa 16, Fc Porto watakipiga dhidi Lyon wakati Real Betis watawakaribisha Eintracht Frankfurt