Taasisi ya ustawi wa jamii yatoa elimu na msaada

0
220

Watumishi Wanawake wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii iliyo chini ya wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum kupitia kituo chake cha elimu, ushauri na msaada wa kisaikolojia wametembelea shule ya sekondari ya Mugabe na shule ya msingi Mapambano zote ‘za mkoani Dar es Salaam, kwa lengo la kutoa elimu kwa Wanafunzi juu ya mahusiano, maadili na uraibu wa dawa za kulevya na vilevya.

Wanawake hao pia wametembelea kituo cha Watoto yatima na Watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Faraja kilichopo Mburahati wametoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani