Kundi la mwisho la Watanzania laondoka Sumy

0
684

Kundi la mwisho la Wanafunzi 32 wa Kitanzania waliokwama katika mji wa Sumy nchini Ukraine, limeondoka kwa mabasi kuelekekea kwenye miji ya Portavo na Lviv nchini humo na kuingia katika nchi ‘za Hungary na Poland.

Hatua hiyo imefikiwa baada kufanyika kwa mazungumzo kwa njia ya simu baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Liberata Mulamula na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba.

Wakati wa mazungum’zo hayo, Tanzania iliiomba Ukraine kusaidia kuwatoa Watanzania wanaosoma katika chuo cha Sumy.

Naibu Waziri Kuleba aliridhia ombi la kuwasaidia Watanzania kuondoka Ukraine salama kupitia mipaka ya nchi za Poland na Hungary kwa utaratibu ulioratibiwa na ubalozi wa Tanzania katika nchi za Sweden, Ujerumani na Russia na kusimamiwa na uongozi wa chuo cha Sunny.