Yanga yaondoka na dhahabu za Geita Gold FC

0
1547

Yanga SC imeondoka na alama tatu kutoka Uwanja wa CCM-Kirumba, Mwanza baada ya kuwaadhibu matajiri wa dhahabu, Geita Gold FC kwa goli 1-0.

Ushindi huo unaimarisha nafasi ya Yanga kileleni ikiwa na alama 45, huku Geita Gold ikiwa na 21 baada ya timu zote kucheza michezo 17.

Goli la Yanga limefungwa na Fiston Mayele dakika ya kwanza ya mchezo, na kudumu kwa dakika 90 za mchezo.

Yanga inaendeleza wimbi la ushindi ambapo kati ya michezo hiyo, imeshinda michezo 14, ikienda sare mitatu huku ikiwa haijapoteza mchezo wowote. Kwa upande wa Geita Gold imeshinda michezo mitano, imeenda sare michezo sita na kupoteza sita.