Dkt Mpango aahidi ushiriki wa Tanzania kuifanya Dunia kuwa salama

0
129

Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo tarehe 3 Machi, 2022 ameshiriki katika mkutano maalum wa kuadhimisha miaka hamsini ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) uliofanyika katika makao makuu yake Jijini Nairobi nchini Kenya.

Akiwasilisha salamu za Rais Samia Suluhu Hassan, Dkt. Mpango amesema kuwa Tanzania inayofuraha kushiriki maadhimisho hayo na inawahakikishia utekelezaji pamoja na kuiunga mkono UNEP katika majukumu yake yakuifanya dunia kuwa salama kwa wote.

Makamu wa Rais amesema kuwa Tanzania inathamini juhudi ya Shirika la Mazingira Duniani kuwa mstari wa mbele katika kutetea mabadiliko ya tabia nchi, kupotea kwa bioanuai, pamoja na uchafuzi wa mazingira.

Amesema kuwa Shirika la Mazingira Duniani UNEP, limeonesha uongozi madhubuti kwa kushirikisha wajumbe katika kukabiliana na masuala ya mazingira na unahitajika ushirikiano wa pamoja

Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo tarehe 3 Machi, 2022 ameshiriki katika mkutano maalum wa kuadhimisha miaka hamsini ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) uliofanyika katika makao makuu yake Jijini Nairobi nchini Kenya.

Akiwasilisha salamu za Rais Samia Suluhu Hassan, Dkt. Mpango amesema kuwa Tanzania inayofuraha kushiriki maadhimisho hayo na inawahakikishia utekelezaji pamoja na kuiunga mkono UNEP katika majukumu yake yakuifanya dunia kuwa salama kwa wote.

Makamu wa Rais amesema kuwa Tanzania inathamini juhudi ya Shirika la Mazingira Duniani kuwa mstari wa mbele katika kutetea mabadiliko ya tabia nchi, kupotea kwa bioanuai, pamoja na uchafuzi wa mazingira.

Amesema kuwa Shirika la Mazingira Duniani UNEP, limeonesha uongozi madhubuti kwa kushirikisha wajumbe katika kukabiliana na masuala ya mazingira na unahitajika ushirikiano wa pamoja hususan katika sekta ya teknolojia ili kupunguza gharama za nishati mbadala pamoja na kulinda vyanzo vya maji

Makamu wa Rais amesisitiza kwamba suala la utunzaji mazingira linapaswa kupewa kipaumbele ili kuwa na dunia salama kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Aidha Makamu wa Rais amesema Tanzania imekua ikifanya jitihada za kukabiliana na uchafuzi wa mazingira unaotokana na taka za plastiki

Fauka na hayo Dkt. Mpango amesema juhudi za pamoja zinahitajika katika kukabiliana na taka ngumu, taka uoevu na uchafuzi wa mazingira kwa ujumla hususani kupitia taka za plastiki.

Dkt. Mpango amesema kuwa Tanzania ipo mstari wa mbele katika uhifadhi wa mazingira ikiwemo kuanzisha kampeni ya kupanda miti nchi nzima, utunzaji wa bioanuai, kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala, pamoja na utunzaji wa vyanzo vya maji.

katika sekta ya teknolojia ili kupunguza gharama za nishati mbadala pamoja na kulinda vyanzo vya maji