Naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi Atupele Mwakibete ametoa mwezi mmoja kwa wakala usimamizi wa meli TPA na shirika la bima ya taifa NIC kuhakikisha wananunua injini Mpya kwa ajili ya meli ya Mv mbeya II iliyoharibika injini siku chache zilizopita
Mwakibete ametoa agizo Hilo Mara baada ya kutembelea bandari ya kiwira ambako meli hiyo imepaki kutokana na kuharibika injini siku chache baada ya kutengenezwa na Songolo Marine ya mkoani Mwanza
Amesema serikali imetumia pesa nyingi Sana katika kuzijenga meli hizo tatu ya Mv mbeya II ,Mv ruvuma na Mv Njombe ambazo zimeegeshwa kutokana na kukosa mzigo wa kusafirisha kwa njia ya maji