Dkt Mpango ashiriki ibada ya Jumatano ya majivu Nchini Kenya

0
137

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akiongozana na mkewe Mama Mbonimpaye Mpango leo tarehe 2 Machi 2022 wakiwa Jijini Nairobi wameshiriki Ibada ya Jumatano ya majivu katika kanisa la Mtakatifu Paulo mtaa wa chuo kikuu cha Nairobi.

Akiongoza Ibada hiyo Paroko msadizi wa Kanisa katoliki la Mtakatifu Paulo Padre. Edwin Hunja amewataka waumini kutumia kipindi hiki cha kwaresma katika kutafuta msamaha na huruma ya mwenyezi Mungu pamoja na kujielekeza kutenda matendo yaliyo mema. Padri Paulo amesema mwezi huu wa Kwaresma unapaswa kutumika katika kuwapatanisha wale wanaofarakana na kombea dunia kuwa sehemu ya Amani.

Ibada ya majivu kwa waumini wa Imani ya kikristo ni mwanzo wa mfungo na kipindi cha kwaresma kuelekea sikukuu ya pasaka.