Mtuhumiwa wa usafirishaji wa Mirungi akamatwa

0
168

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limemkamata Elia Mbwambo (45) mkazi wa Ngaramtoni akiwa anasafirisha madawa ya kulevya yanayodhaniwa kuwa mirungi yenye uzito wa 187kg.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo amesema tarehe Tarehe 01.03.2022 muda wa 06:30 mchana huko maeneo ya Ngaramtoni, Mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa anasafirisha madawa hayo kwa kutumia gari lenye namba za usajili T.793 CUY aina Varian.

Amesema kuwa Uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akijihusisha na biashara hiyo haramu ya usafirishaji wa dawa za kulevya katika maeneo mbalimbali jijini Arusha.

Ameendelea kusema kuwa mara baada ya upelelezi kukamilika jalada litapelekwa ofisi ya taifa ya mashtaka kwa ajili ya kulitolea maamuzi kisheria.

ACP Masejo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa Jeshi la Polisi ili kutokomeza kabisa uhalifu ndani ya mkoa wetu. Pia niwatake baadhi ya watu wachache wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya kuacha mara moja tabia hiyo kwani hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi yao.