Marubani wa Helikopta za Kijeshi waongezeka

0
213

Wizara ya ulinzi na Jeshi la kujenga taifa imesema kumekuwa ongezeko kubwa la marubani wa Helikopta za kijeshi watakaotumika kutoa huduma kwa jeshi na mamlaka za kiraia.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa , Dkt. Stergomena Lawrence Tax ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kutunuku Leseni (Commercial Pilot Licence) na Log Book kwa marubani wapya wa Helikopta 20 katika uwanja wa Ndege na Usafirishahi Jijini Dar es Salaam.

Aidha Dkt.Tax amesema Wizara anayoiongoza itaendelea kutoa mafunzo kwa marubani wengi na kuwawezesha kufanya kazi zao kwa weledi kwa Jeshi na Taifa kwa ujumla.