Kikwete: Tutengeneze sera zinazotabirika kwa wawekezaji

0
169

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete ameitaka wizara ya madini kuwa na sera zinazotabirika kwa wawekezaji ili kuongeza tija na kuongeza idadi ya wawekezaji katika sekta ya madini

Rais Mstaafu Dkt. Kikwete amezungumza hayo wakati akitoa hotuba yake katika usiku wa madini uliofanyika jijini Dar es salaam mara baada ya Mkutano wa Kimataifa wa uwekezaji wa sekta ya Madini nchini uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere

Aidha Rais Mstaafu Dkt. Kikwete amesema “Nchi yetu imebarikiwa kuwa na rasilimali mbalimbali ikiwemo madini na takribani madini yote yanayotajwa duniani yanapatikana hapa nchini”

Fauka na hayo Rais Mstaafu Dkt. Kikwete amempongeza Rais wa awamu ya sita, Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuyapa thamani madini yetu na kutengeneza sera zitakazoiwezesha sekta hiyo kuchangia pato kubwa kwa taifa

Katika halfa hiyo Rais Mstaafu Jakaya Kiwete aliambatana na mkewe Mama Salma Kikwete na kutoa wito kwa wazawa kuwekeza katika sekta ya madini ili kujiongezea kipato na kutengeneza fursa za ajira kwa Watanzania