tutamaliza upungufu wa Chumvi

0
2641

Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko amesema Wizara inaendelea na jitihada za kumaliza upungufu wa chumvi nchini ambapo uhitaji ni tani laki 2.5, lakini inayozalishwa nchini ni tani laki 1.2.

Amesema kwamba kama ambavyo iliwezekana kuzalisha makaa ya mawe ya kutosha hapa nchini, watafanya hivyo pia kwa chumvi.

Aidha, amesema wizara kwa kushirikiana na wadau wengine watahakikisha sekta hiyo inakua na kufikisha  asilimia 10 ya mchango wake kwenye Pato la Taifa kutoka asilimia 7.9 ya sasa.