Makalla awapa ‘Tano’ DAWASA

0
114

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla, ameipongeza mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), kwa kuokoa maji yaliyokuwa yakipotea bila kufika kwa watumiaji kutokana na miundombinu mibovi na chakavu.

Makalla ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya 16 ya siku ya Bonde la Mto Nile yaliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City Dar es Salaam huku mgeni rasmi akiwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.

Makalla amesema miaka ya nyuma hali ya upatikanaji wa Maji katika mkoa wa Dar es Salaam ilikuwa tabu lakini kwa uchapa kazi wa Waziri wa Maji Jumaa Aweso maeneo mengi kero ya maji imepungua.

Kwa upande wa matumizi ya maji taka amesema kutakuwa na miradi mikubwa mitatu na mingine midogo midogo itakayohudumia wananchi wa Dar es Salaam na kusaidia utunzaji wa mazingira.