Mto Nile ni uhai wa waafrika

0
107

Waziri wa Maji Tanzania Jumaa Aweso, amesema asilimia kumi ya wananchi barani Afrika wanategemea maji kutoka bonde la mto Nile kwa shughuli za kila siku hivyo ni muhimu kwa nchi wanachama wa bonde hilo wakashikamana ili kutunza vyanzo vya bonde hilo.

Waziri Aweso ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya 16 ya siku ya bonde la mto Nile yaliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City Dar es Salaam.

Katika hotuba yake Aweso amesema Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, itaendeleza juhudi na ushirikiano kwa mataifa yote wanachama ya bonde la mto Nile ili kulinda usalama wa mto huo na kunufaisha vizazi vijavyo.

Aweso amesema njia pekee ya kulinda bonde hilo ni sekretarieti ya umoja huo kushirikiana kwa umoja wao kulinda bonde hilo ambalo Mungu aliamua kuliweka Afrika badala ya Bara lingine Dunia.

Katika hatua nyingine waziri Aweso ameshauri katika vikao na mikutano ya umoja huo itumike lugha ya kiswahili kwani kimezidi kukua barani Afrika na kimekuwa na wadau wengi.