Makamu wa Rais ahimiza kufaidika na rasilimali ya Maji kwa Amani

0
158

Makamu wa Rais Dkt. Phillip Mpango, amesema umakini, utashi na kuaminiana kutumike katika kutafuta namna bora ya kutumia rasilimali ya maji ya bonde la mto Nile ili isiwe chanzo cha migogoro baina ya nchi wanachama.

Akizungumza katika kilele cha Maadhimisho ya 16 ya Bonde la Mto Nile yanayofanyika Dar es salaam Dkt. Mpango amesema idadi ya watu wanaotumia maji ya bonde hilo imefikia zaidi ya watu milioni 300 ni muhimu nchi wanachama wakaweka mipango ya pamoja ili manufaa ya mto huo yasilete migogoro baina yao.

Naye Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Ivu Bazaiba akizungumzia umuhimu wa mto Nile amesema umetumia kuziunganisha nchi, viongozi wajitahidi bonde hilo lisiwe chanzo cha migogoro baina ya nchi wanachama wa bonde hilo.

Pia Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Mafredo Fanti amesema nchi zilizopo katika Ukanda wa Mto Nile zinawajibu wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia nchi ili kuhifadhi vya maji ya mto huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Maaendeleo la Marekani USAID Kate Somvongsiri amesema serikali yake ipo Tayari kuendelea kusaidia wadau wa Maendeleo ili kuhifadhi vyanzo vya maji sambamba na kushughulikia changamoto zinazolikumba bonde la mto Nile zikiwemo ongezeko la matumizi ya maji ya mto huo inayosababishwa na kuongezeka kwa Idadi ya watu.