Ufaransa na Ubelgiji kumulika fursa za uwekezaji nchini

0
156

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amerejea nchini leo baada ya kufanya ziara yake katika nchi za Ufaransa na Ubelgiji.

Akizungumza na wakazi wa Dar Es Salaam waliojitokeza kumlaki kwa wingi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal I), Rais Samia amesema ziara hiyo imekuwa yenye mafanikio makubwa katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, uchumi na kutanua sekta nyingine mtambuka za maendeleo.

Pia, Rais amesema mikataba yote iliyosainiwa na misaada ya kifedha iliyopatikana italeta tija kubwa katika kuchechemua shughuli za maendeleo.

Rais amedokeza kwamba wawekezaji kutoka mataifa ya Ufaransa na Ubelgiji watafika nchini Tanzania kumulika na kuangalia fursa za uwekezaji zilizopo.

Kiongozi huyo Mkuu wa Nchi amekuwa ziarani kwa juma moja katika ziara inayotajwa kuwa yenye mafanikio makubwa katika mkondo wa kidiplomasia na kiuchumi.