Tanzania yaingia 10 bora kwa uzuri wa asili duniani

0
124

Tanzania imeshika nafasi ya nne (4) kwa uzuri na kuingia katika kundi la nchi kumi (10) zilizotajwa kwa uzuri zaidi wa asili duniani.

Kwa mujibu wa ripoti ya dunia kuhusu uzuri wa asili (Natural Beaty Report) iliyotolewa na tovuti ya uingereza ya Money.co.uk ambayo ilikusanya takwimu na taatifa za wasafiri imeorodhesha Tanzania kwa kupata lama 6.98 kati ya kumi.

Vipengele vilivyoipelekea Tanzania ishike nafasi ya nne ni pamoja na kuwa na mandhari nzuri za asili ikiwemo milima mashuhuri ya Volcano kama Kilimanjaro ambao ni mlima mrefu zaidi Afrika,Mlima Meru na Oldonyo Lengai pamoja na misitu asilia mingi.

Pia eneo la kreta ya Ngorongoro lenye utajiri mkubwa wa asili, hifadhi ya taifa Serengeti yenye uwanda mpana na bora zaidi duniani iliyojaa wanyama pori wakibwa na wadogo wa kuvutia, spishi mbalimbali za ndege na mimea ni sababu zilizoiwezesha Tanzania kuingia kwenye kumi bora duniani.

Sababu nyingine ni uwepo wa eneo lenye miamba ya matumbawe lenye kilometa za mraba 3,580 na uwepo wa maeneo mengi yaliyohifadhiwa yenye jumla ya kilometa za mraba 307,873

Katika mashindano hayo, Indonesia imetwaa taji la kwanza kwa kupata alama 7.77 ikifuatiwa na New Zealand 7.27, Colombia 7.16, Tanzania 6.98, Mexico 6.96, kenya ikishika nafasi ya 6 kwa kupata alama 6.7.

Nchi nyingine ni India nafasi ya saba, ufaransa nafasi ya nane, Papau Guinea nafasi ya tisa huku Comoro ikishika nafasi ya kumi.