Dkt. Mwinyi ampongeza Mke wake kusaidia wananchi

0
234

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amempongeza mke wake Maryam Mwinyi kwa kuanzisha taasisi ya kusaidia wananchi katika Nyanja mbalimbali za maendeleo.

Dkt. Mwinyi amepiga simu katikati ya hafla hiyo na kuelezea namna alivyofurahishwa na hatua ya kuanzishwa kwa taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) na kuahidi kuwa serikali yake itashirikiana na taasisi hiyo katika kuwahudumia wananchi.

“Nampongeza kwa dhati Mke wangu Bi Maryam Mwinyi kwa kiuanzisha taasisi hii ambayo itakuwa na kazi ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia katika jamii lakini pia kuwaletea maendelea wananchi” amesema Dkt. Mwinyi

Dkt. Mwinyi pia amewataka wadau wa maendeleo waliofika katika hafla hiyo kuendelea kuiunga mkono taasisi hiyo ili itekeleze kwa ufanisi malengo yake.

Kwa upande wake Mke wa Rais wa Zanzibar, Maryam Mwinyi amesema lengo kuu la kuanzishwa kwa ZMBF ni kuwainua wananchi kiuchumi na kimaendeleo na pia kupambana na unyanyasaji wa kijinsia.

Taasisi Zanzibar Maisha Bora foundation imezinduliwa hii leo na itakuwa ikifanya kazi mbalimbali za maendeleo kwa wanchi ikiwa ni pamoja na kushirikiana na serikali katika kuwahudumia wananchi.