Spika akabidhiwa makombe saba

0
2084

Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson leo amekabidhiwa makombe saba ambayo timu za bunge zilishinda katika mashindano ya mabunge Afrika Mashariki yaliyofanyika jijini Arusha Desemba 2021.

Katika mashindano hayo bunge la Tanzania liliibuka bingwa wa jumla baada ya kubeba makombe saba katika michezo tofauti.

Makombe ambayo Tanzania ilishindi ni katika michezo ya pete, kikapu kwa wanaume na wanawake, wavu kwa wanaume na wanawake, mpira wa miguu na kuvuta kamba kwa wanaume.

Katika taarifa yake, uongozi wa timu ya bunge umeahidi kwamba utaendelea kufanya mazoezi kujiweka sawa, ili mashindano yoyote watakayoshiriki waweze kuiwakilisha nchi vizuri.

Hafla ya kukabidhi makombe hayo imefanyika katika viwanja wa Bunge jijini Dodoma.