Mwili wa Dkt. Mwele kuwasili Ijumaa

0
172

Familia ya Waziri Mkuu Mstaafu John Malecela imesema mwili wa Mpendwa wao Dkt. Mwelecele Malecela utawasili Dar es salaam Ijumaa ya Wiki hii majira ya saa 5 usiku katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere.

Baada ya kupokelewa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Mwili huo utapelekwa Upanga Sea View nyumbani kwa Mzee Malecela ambapo utalazwa hapo.

Jumamosi asubuhi itafanyika sala fupi nyumbani Sea View na kisha mwili utapelekwa Kanisani na kisha Karimjee kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho na kisha jioni utasafirishwa kuelekea Dodoma kwa ajili ya taratibu za mazishi.