Mondi na Zari ndani ya series moja

0
3168

Netflix wako njiani kuzindua ‘series’ yao ya kwanza ya kiafrika ihusuyo maisha ya uhalisia ya washiriki wake iitwayo Young, Famous & African.

Series hiyo itawajumuisha watu maarufu kutoka Afrika wakiwemo Khanyi Mbau, Nadia Nakai, Annie Macaulay-Idibia na mumewe Innocent Idibia ama 2baba, Kayleigh Schwark, Andile Ncube, Swanky Jerry, Diamond Platnumz kutoka Tanzania pamoja na mama watoto wake Zari the Boss Lady.

Netflix imetangaza kuwa show hiyo itaruka rasmi Machi 18, mwaka huu ikionesha maisha ya mastar hao ya kazi na nje ya kazi, habari zao zilizozungumziwa sana mitandaoni na namna wanavyoweza kuishi ndani ya umaarufu waliojizolea.