Zungu achaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge

0
235

Mussa Zungu, Mbunge wa Ilala, Dar es Salaam na kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) amechaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Tanzania.

Zungu ambaye alikuwa mgombea pekee kwenye uchaguzi huo, ameshinda baada ya kupata kura 296 (98.33%) za NDIYO, huku kura za hapana zikiwa 3, na kura zilizoharibika ni 2.

Kabla ya uchaguzi wa leo Zungu alikuwa mmoja wa wenyeviti wa Bunge, nafasi ambayo ameitumikia tangu mwaka 2012 alipochaguliwa kwa kipindi cha kwanza.

Wakati akiwa mbele ya Bunge kuomba kura, ameahidi kufanya kazi kwa kuzingatia majukumu ya Naibu Spika yaliyoainishwa, pamoja na maelekezo atakayopewa na Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.

Nafasi ya Naibu Spika wa Bunge ilikuwa wazi kufuatia kujiuzulu kwa Dkt. Tulia Ackson Januari 31, 2022 ili aweze kugombea nafasi ya Spika wa Bunge.