Majaliwa: Tunaliangalia suala la mabasi kusafiri usiku

0
200

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekiri kuwa kuna uhitaji wa kuruhusu mabasi ya abiria kufanya safari zake usiku ili kukuza biashara.

Akijibu swali la mbunge aliyesema kwamba zuio hilo liliwekwa bila msingi wa sera au sheria, na kutaka kujua kwa nini serikali isiruhusu mabasi kufanya safari zake ili kukuza uchumi ikiwa sasa Tanzania ni nchi ya uchumi wa kati, na kutokana na kuimarika zaidi usalama.

Licha ya umuhimu huo, Waziri Mkuu amesema kwamba majadiliano yanahitaji kufanyika mamlaka zinazohusika ili kuona uwezekano wa utekelezaji wake.

Ameongeza kwamba serikali imejidhatiti kuhakikisha kwwamba biashara zinafanyika kwa saa 24, ikiwa ni pamoja na kuwa na maduka ambayo watu ambao wanakuwa ‘busy’ wakati wa mchanga, wanaweza kufanya manunuzi wakati wa usiku.