Mkoa wa Mara una utajiri wa Utalii

0
228

Waziri wa Maliasili na Utalii Damas Ndumbaro ameutaja Mkoa wa Mara kama Mkoa wenye utajiri wa Utalii kutokana na vivutio vyake.

Ndumbaro amesema Mkoa huo una vivutio ambavyo ni bora huku vingine vikiongoza kwa ubora katika bara la Afrika.

Ndumbaro ameyasema hayo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alipokuwa akitoa salaam za Wizara yake katika hafla ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa mradi wa maji wa Mgango, Kiabakari, Butiama.

Amesema Wizara yake kwasasa inautazama Mkoa wa Mara kwa jicho la tatu ili kuendelea kulinda na kuendeleza vivutio vilivyopo.

Akitolea mfano hifadhi ya Serengeti ambayo imekuwa hifadhi bora barani Afrika kwa mara tatu mfululizo, amesema hifadhi hiyo imekuwa chachu ya maendeleo Nchini kutokana na Watalii wengi kutembelea mbuga hiyo.

Amewaasa Wananchi kuendelea kulinda na kuvitunza vivutio hivyo kwa maslahi mapana ya vizazi vijavyo.