Mameneja TARURA kutoa taarifa kila mwezi

0
155

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amemuagiza Katibu Mkuu TAMISEMI kuhakikisha Mameneja wa TARURA wa mikoa yote nchini wanatoa ripoti kila mwezi kuhusu kazi zao kwa kuwa moja ya kigezo cha kuwapima ni utendaji kazi uliotukuka.

Bashungwa ametoa agizo hilo leo kwenye uwekaji wa jiwe la msingi kwenye Mradi wa Majisafi wa Mugambo-Kiabakari-Butiama katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma mkoani Mara.

Amesema kazi ya Mameneja Mikoa ni kuhakikisha fedha zinazotolewa na Serikali katika ujenzi wa miundombinu ya barabara zinasimamiwa kwa weledi na kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana kwenye ubora wa miundombinu ya barabara inayotekelezwa.

Bashungwa amesema Ofisi ya Rais – TAMISEMI inaendelea kufanya maboresho kwa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) ili iweze kusimamia kikamilifu fedha zinazotolewa na Serikali katika ujenzi ya miundombinu ya barabara nchini ili kuwafungulia wananchi barabara za vijijini na kufika kusikofikika.