Dkt. Chaula azifunda AZAKI juu ya kufuata sheria

0
244

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Zainab Chaula amekutana na kufanya kikao na Asasi za Kiraia (AZAKI) kutoka mikoa ya Dodoma, Singida na Iringa kujadiliana juu ya ustawi wa taasisi hizo nchini.

Dkt. Chaula ameeleza kuwa kikao hicho pamoja na mambo mengine kimelenga kupokea changamoto, kutoa elimu ya namna ya kuendesha AZAKI kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu na kukubaliana namna ya kuimarisha sekta hiyo.

Washiriki wa kikao cha AZAKI mkoani Dodoma

Ameongeza kuwa kikao hicho kimetoa fursa kwa AZAKI kutoka mikoani kutoa maoni yao na kupata uwakilishi katika vikao na wizara.

Asasi hizo zimekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Tanzania ambapo zimekuwa zikitoa elimu kwa wananchi kuhusu mipango mbalimbali ya serikali ikiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi, masuala ya kiafya na demokrasia.

Mbunge Neema Lugangira

Akizungumza kwenye kikao hicho Mbunge Neema Lugangira ambaye ni mmoja wa wadau wa AZAKI ameishukuru wizara kwa kukutana na taasisi hizo, na kuongeza kwamba ushirikiano wa karibu kati ya serikali na asasi za kirai utawanufaisha wananchi wote.