Makamu wa Rais kumuwakilisha Rais AU

0
236

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango ameondoka nchini hii leo kuelekea mjini Adis Ababa, Ethiopia kumuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa 35 wa wakuu wa nchi na serikali wa Umoja wa Afrika (AU).

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Februari 5 na 6 na utajadili mambo mbalimbali yanayohusu Bara la Afrika huku kauli mbiu ikiwa ni kuimarisha lishe na usalama wa chakula: Kuongeza kasi katika uzalishaji wa Kilimo, maendeleo ya rasilimali watu na maendeleo endelevu ya kiuchimi na kijamii.

Mkutano wa wakuu na nchi na Serikali unafanyika baada ya mkutano mwingine wa Mawaziri wa mambo nje wa nchi hizo kufanyika Februari 2 na 3, mjini Adis Ababa.