Soko la Buguruni kuendelea kuimarishwa ili kulinda hali ya usalama wa Chakula

0
187

Shirika la Global Alliance for Improved food Nutrition (GAIN), kupitia mradi wa kuwezesha masoko kuzalisha katika hali ya usalama wamefanya kikao na wadau, chenye lengo la kuwasilisha matokeo ya tafiti zilizofanyika juu ya mtazamo wa wauzaji na wanunuzi katika masoko hususani soko la Buguruni kuhusu Usalama wa Chakula ( Safe food ) sokoni.

Akiongea wakati wa Kikao hicho Meneja wa mradi Edwin Josiah amesema kabla ya kikao hicho wamepata wasaa wa kutembelea na kujionea Uhalisia kwa sasa katika Soko la Buguruni na kuongea na wafanyabiashara kusikia maoni na ushauri, hivyo kikao kilichofanyika kimetoa fursa kwa wadau kwa pamoja kujadili namna bora ili kufikia adhima ya usalama wa chakula katika masoko likiwemo soko hilo.

Kwa upande wake Meneja wa Soko hilo Seleman Mfinanga, amesema Shirika la GAIN limekua mdau mzuri katika kufikia Usalama wa Chakula katika Soko la Buguruni kwa kufadhili Ukarabati mkubwa wa Soko kuanzia kuweka Sakafu, kuezeka paa sehemu ya kina mama lishe, Kuboresha sehemu ya mchinjio ya kuku, Kuwapa majiko ya gesi kwa kina mama lishe ili waachane na matumizi ya mkaa.

Mwisho kikao kazi hicho kimehudhuriwa na wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Ofisini ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala ,Viongozi wa Soko la Buguruni pamoja na Wafanyabiashara na Wataalam kutoka Shirika la GAIN ( Global Alliance for Improved food Nutrition).