Timu ya Taifa ya Senegal imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuichapa Burkina Faso 3-1 katika mchezo wa Nusu Fainali usiku wa Jumatano Uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaoundé nchini Cameroon.
Mabao ya Senegal yamefungwa na Abdou Diallo dakika ya 70, Bamba Dieng dakika ya 76 akimalizia kazi nzuri ya Nahodha, Sadio Mane ambaye naye alifunga la tatu dakika ya 87.
Bao pekee la Burkina Faso limefungwa na Blati Toure dakika ya 82 na sasa Senegal itakutana na mshindi kati ya wenyeji, Cameroon na Misri wanavaana leo katika Nusu Fainali ya pili.