Urusi: Marekani mchochezi

0
235

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameishutumu Marekani kwa kujaribu kuiingiza nchi yake kwenye vita na Ukraine.

Amesema lengo la Marekani lilikuwa kutumia mvutano huu kama kigezo cha kuweka vikwazo zaidi kwa Urusi.

Putin pia amesema Marekani imekuwa ikipuuzia wasiwasi uliyotolewa na Urusi kuhusu kuongezeka kwa vikosi vya NATO barani Ulaya.

Marekani na Muungano wa NATO unaishutumu Urusi kupanga kuivamia Ukraine huku Urusi ikikana mara zote.

Wakati huo huo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa onyo kwa Urusi akisema uvamizi wowote wa nchi hiyo hautaishia kuwa vita kati ya Ukraine na Urusi bali vita kubwa na kamili ndani ya bara lote la Ulaya.