Zuhura Yunus Mkurugenzi Mawasiliano Ikulu

0
169

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Zuhura Yunus Abdallah kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu

Kabla ya uteuzi huo alikuwa mtayarishaji wa vipindi na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

Zuhura Yunus anachukua nafasi ya Jaffar Haniu ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Uteuzi huo umeanza tarehe 30 Januari 2022.