Chongolo awasili Busega

0
133

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo, amewasili na kupokelewa kwenye uwanja Kilole, wilaya ya Busega mkoani Simiyu tayari kwa ziara kukagua, kuhamasisha na kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025 pamoja na kukagua uhai wa Chama katika ngazi za mashina.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu ameongozana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.