Meli ya Mv Mbeya II yaanza tena safari baada ya miezi 9

0
189

Meli ya Mv Mbeya II leo imeanza kufanya safari zake mkoa wa Ruvuma na Njombe baada ya kupata hitilafu miezi tisa iliyopita ikiwa na abiria zaidi ya mia moja na hamsini.
.
Akizungumza Katika uzinduzi wa meli hiyo ambayo tayari imepewa cheti na taasisi ya udhibiti wa vyombo vya maji TASAC,Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari ya Itunge Abdalah Mohamed, amesema tayari matengenezo yamekamilika kwa asilimia mia moja na utoaji huduma utaendelea.

Amesema meli hiyo ilipata hitilafu iliyotokea wakati wa dhoruba mwezi Machi mwaka 2021 ilipokuwa ikitia nanga katika bandari ya Matema.

Awali akizindua safari za meli meli hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera, amesema Serikali imetumia zaidi ya Bilioni tisa kufanya matengenezo ya meli hiyo itakayokuwa mkombozi kwa wakazi wa wilaya na mkoa huo waliokosa huduma hiyo kwa muda mrefu.

Amewataka wafanyakazi wa meli hiyo kuwa waaminifu na wazalendo katika kutoa taarifa pale wanapobaini kuna uharibifu ndani ya meli hiyo.

Baadhi ya abilia walioanza safari wameishukuru serikali kwa kufanya ukarabati huo na kupata ahueni ya usafirishaji wa bidhaa zao ambapo awali ulitumia alikuwa wakitembe a umbali mrefu