Walioshiriki mauaji Kilindi kusakwa usiku na mchana

0
175

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Tanga Adam Malima, amesema atahakikisha kila aliyeshiriki kwenye mauaji wa watu saba wilayani Kilindi anashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Mwenyekiti huyo ametoa kauli hiyo mara baada ya kutembelea kijiji cha Kibirashi wilayani humo mahali ambapo yametokea mauwaji hayo January 30, 2022.

Amesema Serikali haitakubali kuona wananchi wake wanateseka kutokana na upotevu wa amani unaofanywa na baadhi ya watu.

“Nasema serikali hailali ipo macho muda wote na tutahakikisha sheria inachukua mkondo wake,”- amesema Adam Malima.

Mpaka sasa waliofariki dunia ni watu saba wakiwemo wawili wa familia moja,ambao ni mama na mtoto wa miaka kumi.