Simbachawene ateta na watumishi wa ofisi ya wakili Mkuu

0
122

Waziri wa katiba na sheria George Simbachawene ameiagiza ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kuhakikisha inaendesha mashauri kwa kuzingatia haki ili kuleta tija kwa taifa

Simbachawene amesema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Menejimenti na watumishi wa ofisi ya Wakili mkuu wa Serikali ambapo amesema Serikali itaendelea kuwekeza katika matumizi ya mfumo wa kidijitali ili kuendesha mashauri kwa haraka na ufanisi zaidi.

Naye Wakili Mkuu wa Serikali Gabriel Malata amesema katika kipindi cha miezi Tisa ofisi yake imefanikiwa kuendesha Mashauri ya usuluhishi 444 pamoja na kuokoa shilingi Bilioni 236.

“Ofisi ya wakili Mkuu kwa unyeti wake ina kazi ya kuisaidia Serikali Katika maswala ya uendeshaji Mashauri na tumeweza kujiimarisha katika uwezeshaji kwa watumishi wetu ili wawe imara zaidi Katika kushughulikia Mashauri hayo” ameongeza wakili Mkuu Malata.