Kagera Sugar yaiadhibu Simba SC Kaitaba

0
1558

Kagera Sugar FC imeondoka Uwanja wa Kaitaba ikiwa na alama tatu baada ya kuifunga Simba SC katika mchezo wa kiporo uliokuwa uchezwe Desemba 22, 2021.

Ushindi wa Kagera unafuta uteja wake kwa Simba ambapo katika mechi tano zilizopita kabla ya mchezo wa leo, Simba ilishinda michezo minne, Kagera ikishinda mmoja.

Kwa ushindi huo, Kagera inapanda hadi nafasi ya 9 ikiwa na alama 16, huku Simba ikibaki nafasi ya pili ikiwa na alama 25 baada ya timu zote kucheza michezo 13.

Katika michezo mitatu iliyopita, Simba imepata alama moja baada ya kutoka suluhu na Mtibwa Sugar FC, huku ikipoteza mchezo dhidi ya Mbeya City FC.

Katika mchezo huo, Hamis Kiiza ambaye ndiye mfungaji wa goli pekee na la ushindi akiingia kutoka benchi, ametolewa kwa kadi nyekundu (baada ya kupewa kadi za njano mbili).

Mei 15 mwaka huu timu hizi zitakutana tena katika mzunguko wa pili wa ligi, ambapo Simba itaikaribisha Kagera Sugar katika Uwanja wa Benjamin Mkapa mkoani Dar es Salaam.