Marekani yatishia kumwekea vikwazo Putin.

0
225

Rais was Marekani Joe Biden amesema anaweza kufikiria kumwekea vikwazo Rais wa Urusi Vladmir Putin yeye mwenyewe kama nchi yake itaivamia Ukraine

Biden amesema kutakuwa na “matokeo mabaya na makubwa” kwa dunia kama Urusi itaisogelea Ukraine ambayo ipo Kusini-Magharibi mwa nchi hiyo

Hatua hiyo ya Biden imekuja wakati mataifa mengine ya magharibi yameendelea kuionya Urusi kuhusu tishio lake la kuivamia Ukraine.

Urusi imeishutumu Marekani na wengine kwa kuongeza mvutano juu ya swala hilo na kukana kuwa na mpango wa kuivamia Ukraine.

Hata hivyo Urusi imeshapeleka wanajeshi karibia 100,000 karibia na mpaka na Ukraine.

Wanadiplomasia kutoka Urusi, Ukraine, Ujerumani, na Ufaransa watakutana mjini Paris kwa ajili ya mazungumzo kuhusiana na mvutano huo.