Mpango wa O3 Plus kutokomeza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vyuoni

0
164

Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imesema itaendelea kutafutia mwarobaini wa vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia ili kutokomeza vitendo hivyo katika jamii.

Hayo yameelezwa mkoani Dar es Salaam na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, Dkt.Dorothy Gwajima wakati wa uzinduzi wa dawati la jinsia kwa elimu ya juu.

Aidha Dkt.Gwajima amebainisha kuwa matukio ya ukatili wa kijinsia yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku huku kundi la wanawake likitajwa kuathirika zaidi.

“Vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kundi la wanawake na watoto yameongezeka kutoka18,270 kwa mwaka 2019-2020 hadi kufikia matukio 20,025 kwa mwaka 2020-2021 hivyo nguvu ya pamoja kuhitajika kuyatokomeza.”-Amesema Dkt.Gwajima.

Mpango huo ambao umeratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO limehudhuriwa na wadau mbalimbali Maendeleo ya jamii wakiwemo wanafunzi wa elimu ya juu kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na UDOM.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa elimu Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga, amesema mpango huo ni umuhimu katika elimu ya juu na katika Vyuo vya kati katika kufanikisha ndoto za wanafunzi.

Mpango huo uoiofadhiliwa wa O3 Plus uoiofadhiliwa na UNESCO unalenga kutatua changamoto zinazohusiana na ukatili wa kijinsia kwa vijana katika Vyuo vya elimu ya juu Kusini mwa Afrika ikiwa ni pamoja nakuwapa elimu ya kukabiliana na magonjwa hasa UKIMWI ili kufikia ndoto zao.