Waafanyabiashara wa Karume wapata ahueni

0
193

Mkuu wa wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija amewataka wafanyabiashara waliopatwa na janga la kuunguliwa na bidhaa zao katika soko la mchikichini karume jijini Dar es salaam kutumia eneo la jirani na ukumbi wa Halmasuri wa DIMPI uliopo nyuma ya soko hilo kuendelea na biashara wakati huu ambao tume inaendelea na uchunguzi

Akizungumza na TBC Ludigija amesema lengo la kuruhusu wafanyabiashara hao kuendelea na biashara kwa muda ni kuwawezesha waendelee kujipatia kipato

Aidha Mkuu huyo wa Ilala na Meya wa jiji hilo Omary Kumbamoto wamewatoa hofu wafanyabiashara hao kuwa hakuna mwekezaji yeyote atakaepewa eneo hilo la soko lililopata janga pa moto