Wengi wajitokeza kushiriki Club Rahaleo Dodoma

0
2520
Jaji Mkuu wa shindano la Club Rahaleo show Innocent Nyanyagwa

Wasanii wengi wamejitokeza katika siku ya kwanza ya usaili wa kusaka vipaji kwenye shindano la Club la leo Show huko mjini Dodoma.

Majaji wa shindano hilo wakiongoza na jaji mkuu Innocent Nganyagwa (Ras Inno) wamekuwa na wakati mgumu wa kuchagua vipaji kutokana na uwezo ulionyeshwa na wasaniii hao.

Usaili huo unafanyika kwa siku mbili mjini Dodoma na baada ya hapo utahamia kwenye jiji la Mwanza mwishoni mwa wiki hii.