FIFA yampa tuzo maalum Ronaldo

0
151

Mshambuliaji nyota wa timu ya taifa ya Ureno anayekipiga katika Klabu ya Manchester United, Cristiano Ronaldo amepewa tuzo maalumu na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kwa kuwa Mchezaji Bora wa muda wote wa timu ya taifa.

Kwamjibu wa rekodi, Cristiano Ronaldo amefunga jumla ya magoli 115 katika mechi alizocheza kwenye timu yake ya taifa.

Mbali na hilo, Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Poland anaekipiga kwenye Klabu ya Buyern Munich, Robert Lewandowski ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka 2021katika tuzo hizo za FIFA.

Wengine waliotwaa tuzo ni Edouard Mendy, Golikipa Bora wa FIFA 2021, Kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwaka.

Aidha, bao la Erik Lamela, alilofunga dhidi ya Arsenal limechaguliwa kuwa bao bora la mwaka 2021.