Droo ya 32 bora michuano ya ASFC yatoka

0
950

Droo ya Azam Sports Federation Cup, (ASFC) imechezeshwa leo ikiwa ni hatua ya 32 bora kwenye mashindano hayo.

Simba ambao ni mabingwa watetezi watakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Dar City kwenye mchezo unaoatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Yanga wao watacheza na Mbao FC mchezo huo nao utachezwa pia Uwanja wa Mkapa na matarajio ya mechi hizo kuchezwa ni kati Januari 27-31 na hatua ya 16 bora inatarajiwa kuchezwa kati ya Februari 12-17.

Pia Biashara United watavaana na Mbeya Kwanza, African Lyon dhidi ya Kagera Sugar, African Sports watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar, KMC dhidi ya Ruvu Shooting, Baga Friends dhidi ya Catamine FC.

Timu nyingine ni Tanzania Prisons vs Rhino Rangers,Mbuni FC vs Lipuli,Pamba FC vs Stand United,Azam FC vs Transit Camp, Coastal Union vs Top Boys, Namungo FC vs Lindi United.
Dodoma Jiji vs Sumbawanga United, Polisi Tanzania vs Ndanda FC na Geita Gold vs Tunduru Korosho ambapo washindi wa hatua hii ya 32 bora wataibukia kwenye 16 bora.