Wataalamu Sekta ya Uvuvi watakiwa kukusanyaji maduhuli ya Serikali

0
132

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amewataka wataalam wa sekta ya Uvuvi kuhakikisha wanakusanya maduhuli ya serikali ili kutimiza lengo la kukusanya bilioni 40 kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Waziri Ndaki ameyasema hayo kwenye kikao cha wataalam wa sekta ya uvuvi kilichojadili hali ya ukusanyaji wa maduhuli ya serikali kupitia sekta ya uvuvi ambapo mpaka sasa sekta hiyo imekusanya bilioni 10 kati ya bilioni 40 zilizolengwa. 

Amesema ni lazima wataalam kuhakikisha wanaongeza usimamizi kwenye maeneo yao ili malengo ya ukusanyaji wa maduhuli yatimie. Ili kuhakikisha malengo ya ukusanyaji maduhuli yanafikiwa Waziri Ndaki amesema vituo vitatakiwa kutoa taarifa ya ukusanyaji wa maduhuli kila wiki ili kama kunakuwepo na changamoto iweze kutatuliwa kwa wakati.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Emmanuel Bulayi amesema kuwa lengo la kuitisha kikao hicho ni kufanya tathmini ya hatua iliyofikiwa katika ukusanyaji maduhuli ya serikali pamoja na hali ya ulinzi na usimamizi wa rasilimali za uvuvi.