Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa manispaa na wakuu wa mamlaka ya mapato nchini kuangalia uwezekano wa kuongeza makusanyo kutoka asilimia kumi na saba hadi asilimia thelathini katika kipindi hiki cha mwaka 2019.
Akizungumza na viongozi hao katika kikao maalum cha utendaji ambacho kilikuwa kinapanga mkakati wa kuongeza makusanyo ya mapato katika mkoa wa Dar es salaam ,Makonda amesema lazima viongozi hao watambue fursa nyingine za ukusanyaji wa mapato ili kuhakikisha yanaleta tija katika ustawi wa maendeleo ya mkoa wa Dar es salaam.
Pia amewataka viongozi hao kuwawezesha vijana kutambua fursa za ajira ambazo zitawawezesha vijana hao kuondokana na umasikini.
Kikao hicho tendaji cha kupanga mkakati wa utafutaji wa fursa mbalimbali za makusanyajo wa mapato kimewashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo watendaji wakuu wa halmashauri,vikosi vya ulinzi na usalama ,maafisa kutoka idara mbalimbali na maafisa kutoka mamlaka ya mapato nchini –Tra.