Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akiagana na Viongozi mbalimbali wa Malawi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kamuzu uliopo Lilongwe, mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa dharura wa wakuu wa nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC). Dkt. Mpango alimuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo.