Msafara wa RC wapata ajali, watu kadhaa wafariki dunia

0
194

Watu kadhaa wamefariki dunia katika ajali ya barabarani iliyotokea kwenye eneo la Chumve wilayani Busega mkoani Simiyu.

Taarifa za awali kutoka mkoani Simiyu zinaeleza kuwa ajali hiyo imehusisha msafara wa mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel ambaye alikuwa kwenye ziara ya kukabidhi miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ajali hiyo imehusisha gari lilokuwa limebeba Waandishi wa Habari ambalo limegongana uso kwa uso na gari ndogo ya abiria aina ya Hiace ambapo waandishi wa habari watano wamefariki dunia papo hapo.