Maambukizi ya Corona yaongezeka

0
157

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya kuhusu ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona, ambapo wiki iliyopita kesi za maambukizi zilikuwa milioni tisa na nusu.

Akitoa ripoti ya wiki kuhusu maambukizi ya virusi vya Corona Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema pamoja na kuongezeka kwa maambukizi, idadi ya vifo imepungua.

Tedros ameongeza kuwa licha ya kirusi Omicron kusambaa kwa kasi na kuwa na madhara madogo ikilinganishwa na kirusi Delta, hakipaswi kupuuzwa katika mikakati ya kupambana nacho.