Namungo yatinga nusu fainali Mapinduzi Cup

0
300

Namungo FC imekuwa timu ya kwanza kutinga nusu fainali ya Mapinduzi CUP yanayoendelea visiwani Zanzibar baada ya kuifunga Yosso Boys magoli 2-0.

Magoli ya Namungo yamefungwa dakika ya 53 na Sixtus Sabilo na Leriant Lusajo dakika ya 90.

Huo ni ushindi wa pili kwa Namungo ambapo katika mchezo wa kwanza ilishinda kwa magoli 2-1 ikiifunga Meli 4 City.

Fainali za mashindano hayo ambayo yanafanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matakatifu ya Zanzibar, itapigwa Januari 13 mwaka huu.