Rais Samia Suluhu Hassan ateua viongozi watatu

IKULU, DAR ES SALAAM

0
167

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Baghayo Saqware kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA).

Dkt. Saqware ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA).

Rais Samia Suluhu Hassan pia amemteua Charles Itembe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Eneo Maalum la Mauzo ya Nje (EPZA).

Kabla ya uteuzi huo Itembe alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania.

Naye Ernest Mchanga ameteuliwa na Rais kuwa Katibu wa Tume ya Pamoja ya Fedha (JFC).

Kabla ya uteuzi huo Mchanga alikuwa Katibu Msaidizi, Fedha na Utawala kutoka JFC iliyo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango.

Uteuzi wa Viongozi hao umeanza rasmi tarehe Moja mwezi huu.