Watakaokiuka taratibu za uchaguzi kukiona

0
162

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Tanga, Suleiman Mzee ameonya kuwa chama hicho hakitamvumilia mwanachama yeyote atakayekwenda kinyume na taratibu na sheria za uchaguzi ndani ya chama hicho, unaotarajiwa kufanyika mwaka huu ikiwa ni pamoja na kuanza kampeni kabla ya wakati.

Mzee ametoa onyo hilo jijini Tanga wakati wa mkutano wake na Waandishi wa habari na kuongeza kuwa kuanza kufanya kampeni kabla ya wakati ni kosa kubwa, kwa kuwa kiongozi bora hajitembezi bali huchaguliwa na Wananchi.

“Kwa kweli tukibaini kuwa umetumia njia zisizo sahihi kutafuta uongozi hatutakuvumilia, tutakachofanya ni kutorudisha jina lako kwenye list ya wagombea ili ushindwe kushiriki uchaguzi.” amesema Mzee

Pia Katibu huyo wa CCM wa mkoa wa Tanga amewataka Watendaji wa chama hicho wa mkoa huo wakati ukifika kuacha kutoa fomu za wagombea kwa upendeleo, kwani ni haki ya kila mwanachama kugombea nafasi ya uongozi.